Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, October 12, 2013

HATIMAYE JAJI HERMY B AUNGANA NA IAN NA JULIANA BAAADA YA ZAHIR ZORRO KUACHIA NGAZI

Hatimaye kitendawili cha kama CEO wa B’Hits Music Group, Hermes Lyimo aka Hermy B atarejea tena msimu huu kama jaji wa shindano la Tusker Project Fame kimeteguliwa. Jaji huyo amerejea tena na anaungana na majaji wenzake, Ian Mbugua wa Kenya na Juliana Kanyomozi wa Uganda.
Judges-Ian-Mbugua-Juliana-Kanyomonzi-and-Hermes-Bariki
Hivi karibuni kulikuwa wasiwasi kuwa huenda nafasi hiyo imechukuliwa na mwanamuziki mkongwe, Zahir Zorro baada ya kuonekana wiki iliyopita wakati wa kuchuja wasanii walioingia kwenye academy ya shindano hilo jijini Nairobi, Kenya.
Akiongea na 100.5 Times, FM wiki hii, Hermy B aliwashauri Watanzania kuwaunga mkono washiriki wanne wanaoiwakilisha Tanzania mwaka huu.
“Watanzania wasifikirie kwamba Jaji wao ndiye atakayewapatia ushindi washiriki wao, ndio wapige kura sasa, kwa sababu ushindi wa watu wengi unatokana na kura na sio jaji, hata Juliana akimwambia you are the best of the best lakini asipopigiwa kura hawezi kushinda,” alisema Hermy B.
Tanzania inawakilishwa na Angella Karashani a.k.a Angel, Tanah, Hisia na Dubson. Mshindi wa mwaka huu ataibuka na kitita cha shilingi milioni 100 na mkataba wa kurekodi wenye thamani ya shilingi milioni 200 za Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages