Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Afya ya Tanzania
Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika Magharibi ambaye ni mkazi
wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na
homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Bwana
Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo tayari
ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari katika
hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya watakaohisiwa
kuwa na ugonjwa huo.
Amesema
sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda ameambukizwa
virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini Benin.
Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania.
Taarifa
hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya Tanzania kukanusha
taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa mmoja wa
Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment