Ally Kiba na T.I.D
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa saa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”
Soudy alipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua.
SOURCE BY: http://millardayo.com
Comments
Post a Comment