Mchungaji Christopher Mtikila akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kesi yake kuahirishwa.
...akiondoka mahakamani kwa usafiri wa bajaj.
Na George Kayala MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele hukumu ya kesi ya kuchapisha na kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.
Kusogezwa mbele kwa hukumu hiyo kunatokana na hakimu, Ilvin Mugeta anayesikiliza kesi hiyo kuwa katika majukumu mengine ya kikazi na hivyo hukumu hiyo itasomwa Septemba 6, 2012.
Katika kesi hiyo Mtikila anadaiwa kuwa kati ya Januari 2009 na Aprili 17, 2010 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya uchochezi, alisambaza kwa umma nyaraka zilizosomeka 'Kikwete kuuangamiza ukristo', 'Wakristo waungane kuweka mtu Ikulu'.
Mtikila alikiri kuandaa waraka huo na kusambaza nakala zaidi ya 100,000 nchini, huku akidai kuwa waraka huo si wa uchochezi bali unahusu maneno ya Mungu.
Akiwa mahakamani hapo leo asubuhi, Mtikila amesema anaamini atashinda kesi hiyo kwani hayo yalikuwa ni maoni yake na kila raia ana haki ya kutoa maoni isipokuwa havunji katiba.
Comments
Post a Comment