ZAMARADI MKETEMA ASUMBULIWA NA MWANAE



Mtoto wa host wa Kipindi cha Take One kinachorushwa na Televisheni ya Clouds, Zamaradi Mketema amedai kusumbuliwa na mwanaye.
Akizungumza na paparazi wetu juzi Alhamisi, Zamaradi alidai mwanaye huyo aliyempachika jina la Junior, amekuwa akilia punde anapopelekwa kulazwa kitandani na mtu mwingine.
Alisema kuwa hata kama yeye anatoka kwenda kazini, ni lazima ahakikishe mtoto wake amelala naye mwenyewe kwani ndiye aliyemlaza kinyume na hapo ni kilio mpaka mwisho.
“Yaani Junior ananisumbua sana, akianza kulala analia, akienda kulazwa na mtu mwingine tofauti na mimi ni kilio kikubwa, mpaka anione mimi, tena alale ubavuni mwangu ndiyo amani yake,” alisema Zamaradi.
Pamoja na hayo yote, Zamaradi alisema anahisi furaha mtoto wake kufanya hivyo kwa vile hamchoshi kwani ni ubize anaoufurahia.
Aliongeza kuwa kwa sasa katika maisha yake mambo yake mengi yanaongozwa na uwepo wa mwanye tofauti na zamani ambapo alikuwa akijiamulia mwenyewe.
 “Mambo mengi sana yamebadilika katika maisha yangu ya kila siku, Junior amenifanya kuwa mwanamke shujaa ambaye yuko tayari kupoteza uhai kwa ajili ya mtoto, mwanangu anashika ratiba zangu nyingi kwa siku,” alisema Zamaradi.
 Hata hivyo, Zamaradi alisema siku za karibuni atambatiza mtoto wake huyo ambapo mchakato umeanza kufanywa na baba mtoto ambaye hakutaka kumtaja.

Comments