Mama mzazi wa Sharo Milionea
ana umri wa miaka 52, anasema Hussein maarufu kama Sharo Milionea alikua
mtoto wake wa tatu na wa mwisho, mtoto pekee wa kiume huku wawili
waliomtangulia wakiwa ni wa kike ambao wameolewa tayari.
Taarifa za kifo mama alizipata
akiwa kitandani ameshalala tayari kwenye mida ya saa mbili usiku novembe
26, alianza kupokea simu nyingi za ndugu ambao walikua wanamuuliza tu
vipi Hussein mko nae nyumbani? wote walikua wanamficha lakini baadae
kidogo akaamua kumpigia Sharo Milionea simu ambayo ilipokelewa na mtu
asiemfahamu ambae baada ya kujua aliepiga ni mama Sharo yule mtu alikata
simu, alipopigiwa tena simu ilikua haipatikani.
Mama mzazi amesema Sharo
Milionea hakumwambia kama angekuja Tanga siku hiyo, siku zote ambazo
alikua anakuja Tanga alikua hasemi… alikua anashtukiza tu na mara
nyingine alikua anampigia mama simu na kumwambia “mimi bado niko Dar
wazima huko? baada ya dakika chache tu wanamuona nyumbani Tanga.
Amesema Sharo Milionea alikua
anamtumia kila mwezi shilingi laki moja mpaka laki mbili za matumizi
nyumbani na ameanza kumpa hizo pesa huu ni mwaka wa tatu, mara ya mwisho
kuongea nae kwenye simu ni jumapili iliyopita lakini kuoanana ilikua
mwezi uliopita.
Mara zote hizo walizoongea na
kukutana Sharo hakuonyesha dalili zozote za maisha yake hata mara ya
mwisho kuongea kwenye simu jumapili iliyopita waliongea tu kama kawaida
ambapo Sharo ndio alipiga simu usiku kumsalimia mama yake.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, November 29, 2012
Home
Unlabelled
ALICHOKIONGEA MAMA MZAZI WA SHARO MILLIONAIRE
ALICHOKIONGEA MAMA MZAZI WA SHARO MILLIONAIRE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment