Stori:Haruni Sanchawa
TUKISEMA
staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ yamemkuta ni sawa, kisa
ni ile ishu yake ya kutengeneza filamu inayoitwa Sister Marry ambapo
mapadri wamemtaka asiipeleke sokoni milele, Risasi Jumamosi lina mkanda
wote.
Ishu hiyo ilitokea kwenye kikao kizito cha saa 5 kilichofanyika
Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Washiriki
wa kikao hicho walikuwa Ray, Mkurugenzi Mtendaji wa Utamaduni
aliyetajwa kwa jina moja la Mwansoke, mapadri wanne na mtu mmoja
aliyedaiwa kuwa ni wa kutoka Ofisi za Usalama wa Taifa.
Kikao hicho kilikuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Kanisa
Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam kumtaka msanii huyo ajieleze
kimaandishi ni kwa nini mtawa Sister Marry (Irene Uwoya pichani) alikuwa
akifanya matendo ambayo kiuhalisia, Wakatoliki wenyewe huwa
hawayafanyi.
Kabla Ray hajajieleza kwa maandishi ndipo alipoitwa huko
na kukubaliana ana kwa ana na jopo hilo huku mashinikizo kadhaa
yakielekezwa kwake.
Awali, wajumbe wote wakiwa wamekaa kwenye viti,
filamu hiyo yenye saa 3 iliwekwa mwanzo mwisho huku mapadri hao wakiguna
kila wakati, hasa wakati Sister Marry akiwa anafanya mambo yake mabaya.
Baada
ya kumalizika kwa filamu hiyo, hoja zikaanza. Mwansoke akasema vipande
vyote vichafu vinyofolewe na kubaki vile ambavyo wajumbe hawakuvigunia.
Baada
ya bosi huyo kusema hayo, mapadri wakasema ‘noooo’. Filamu hiyo isiende
mitaani hata kidogo kwani imejaa udhalilishaji wa Wakatoliki.
Inasemekana
Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge Kijijini
(jina halikupatikana mara moja) yeye alipigilia msumari wa mwisho kwa
maneno aliyoyatoa.
Alisema kwa kuwa filamu hiyo ilirekodiwa kwenye
kanisa lake hilo, anataka vipande vyote vya kanisa hilo vitolewe ndipo
iingie mtaani, jambo ambalo lilimtoa machozi Ray.
Ray sasa! Siku ya
Alhamisi iliyopita, Ray alizungumza na gazeti hili na kukiri kuwepo kwa
kikao hicho. Akasema itakuwa vigumu kuviondoa vipande vya kanisa hilo
kwa sababu asilimia 85 ya filamu nzima imerekodiwa Maximilian Kolbe.
“Asilimia
85 ya filamu imerekodiwa Maximilian Kolbe, sasa wanaposema niviondoe ni
kuimaliza filamu yote. Filamu ni ya saa 3, ukivitoa vipande vya kanisa
si itabaki dakika 5 tu,” alisema Ray.
Alisema kikao kiliisha kwa
maamuzi hayo, kwamba mtu wa utamaduni alisema vipande vichafu
vinyofolewe huku mapadri wakitaka muvi nzima isiende sokoni na paroko wa
Maximilian Kolbe akitaka kanisa lake lisionekane kwenye filamu hiyo.
Risasi: “Je, wewe Ray umeamuaje?”
Ray: “Sijaamua chochote kwa kweli. Niponipo tu, nimetumia fedha nyingi sana.”
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, January 26, 2013
Home
Unlabelled
HAYA NDIYO YANAYOENDELEA KUMKUTA RAY JUU YA MOVIE YAKE YA SISTER MARRY
HAYA NDIYO YANAYOENDELEA KUMKUTA RAY JUU YA MOVIE YAKE YA SISTER MARRY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment