Photoafriq ni jarida la bure la mtandaoni ambalo litakuwa likionesha picha za wapiga picha mbalimbali barani Afrika. Toleo la kwanza la jarida hilo lilizinduliwa March 15, 2013 kwenye kituo cha ubinifu wa ICT cha KINU jijini Dar es Salaam.
“Nilianzisha magazine kwasababu nilikuwa naona kwamba wapiga picha wa Tanzania wawe na wanashare pia zao. Kwasababu niliporudi nilikuwa nasoma Malaysia nikawa napiga picha nikaona hamna ile community ya wapiga picha, na kama hamna community ya wapiga picha inakuwa shida kuifanya hiyo industry ikue,” alisema Sinare.
Osse Giovanni Greca Sinare akilizindua Photafriq
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa picha, Sinare anasema, “Picha naongea na photographers na models, sana sana nina page nakuwa napost kwamba unaweza kucontribute so wanakuwa wanacontribute, wanakuwa na guidlines zao. Kwasababu hatuwezi tu kuchukua picha za watu. Na wakitupa images zao tunaweka proper captions, link kwenda kwenye link zao ili wao waweza kupata the maximum coverage.
So far tumepata response nzuri sana. Nimepata photographer wengi Tanzania. Nadhani kwasababu ilikuwa issue ya kwanza after sometime tunaweza kuanza kuona photographers wengine kwenye nchi zingine wanatupa images zao kushare as well. Watu walikuwa wameona kwamba labda magazine ilikuwa haijatoka hawajaweza kuona itaonekanaje, sasa hivi wakiona inaonekanaje wataprove much better kutupa picha zao.
Anazungumziaje changamoto ya internet nchini ambapo watanzania wengi hawana access nayo ili kuweza kusoma jarida hilo la mtandaoni? Sinare anasema, “sasa hivi kusema kweli naona imekua Tanzania lakini percent kama 15 tu ndio inatumia internet.”
Alitolea mfano nchi za Ulaya ambapo watu wengi wana access na internet pamoja na kwenye simu zao kiasi ambacho kiwango cha makato ya internet kimeshuka ukilinganisha na Tanzania ambapo bado yapo juu.
Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo
Sehemu ya kurasa za Photafriq
Kuhusu content itayokuwepo kwenye jarida la Photafriq Sinare anasema, “mwanzoni tulikuwa tunataka tutoe tu picha za photographers, models, stylists na anything to do with photography. Lakini sasa hivi tunabadilisha inakuwa more category based so patakuwa na labda fashion photography, so mpiga picha anakuwa anaweka tu picha za fashion yaani kila aina ya picha.
Alisema jarida hilo amelianzisha kwa makusudi ya kuutangaza uwezo wa wapiga picha wa Tanzania duniani lakini sio mradi anaotegemea kuendesha maisha yake.
“Tukiendelea labda watu watataka kuweka matangazo labda tutakuwa tunachaji, lakini the charging itakuwa ni only to run the magazine sitaki hii magazine iwe sehemu yangu ya mimi kupata hela yangu ya chakula sababu mimi tayari ninayo studio yangu lakini hii ni njia ya to give back to the community of Africa and Tanzania mostly.”
Akizungumzia kama picha za magazine yake ni huru kwa mtu mwingine kuchukua na kutumia, Sinare alisema hairuhusiwi hadi apate ruhusa ya mpigaj i wa picha husika.
“Picha zote zinazowekwa kwenye magazine ziko under copyright ya photographer so all the images is not owned by the magazine zinamilikiwa na mpiga picha aliyeweka picha zake pale.”