Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais wa Jamhuri
ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya ukumbi wa
kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
leo. Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya China na
Tanzania. Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia
picha za matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya
China na Tanzania katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius
Nyerere leo wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar
es Salaam. Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiwa katika
picha ya pamoja na Rais wa China, Mhe. Xi Jinping pamoja na mkewe katika
ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya
sherehe za ufunguzi wa ukumbi huo leo.