Pedaiah Swank John
Pedaiah ni model wa kitanzania anayekuja kwa kasi nchini aliyezaliwa March 7th, 1990. Amehitimu shahada ya Software Engineering mwaka 2012 nchini Malaysia. Ameshafanya matangazo mengi ya biashara ya makampuni makubwa nje na ndani ya nchi. Hivi karibuni alianzisha mavazi yake ya PSJ Couture.
Lengo lake ni kuwa model na mbunifu wa mavazi wa kimataifa.
“My passion is fashion & modelling since childhood after I started my university life that’s when I started working with a number of photographers been enjoying every moment since then. This page showcases some of the work which I have done with different photographers.”
Andrew Mahiga
Andrew Mahiga ana umri wa miaka 26. Ni mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya masuala ya habari, Maanisha Foundation, ambayo lengo lake ni kuwashawishi vijana kubadilisha jinsi wanavyofikiria na kujihusisha kwenye biashara zenye mafanikio.
Maanisha Foundation ina lengo la kuwapa taarifa vijana wa Tanzania ili waamke kutafuta fursa kwaajili ya kujiendeleza wao wenyewe na Tanzania kwa ujumla kupitia televisheni, radio, magazeti na website. Andrew na timu yake wana nia ya kuifanya Maanisha kuwa chombo cha habari chenye magazeti na majarida yake na vipindi vyake vya radio na televisheni.
Tayari wana kipindi chenye mafanikio cha Temino kinachorushwa kupitia Clouds FM. Andrew Mahiga, ana Bachelor of Art – (International Studies) aliyoipata New York , Marekani. Wakati anasoma alifanya field kama mwandishi wa makala za mtandaoni kwenye jarida la Complex Magazine. Ameshafanya kazi pia kwenye kampuni ya Push Observer Media Monitoring.