Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, June 29, 2013

NELSON MANDELA: UJANA MPAKA UZEE

RAIS Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela (94) hali yake kiafya bado tete kwa maradhi ya mapafu na ini yanayomsumbua, hivi sasa amelazwa katika Hospitali ya Mediclinic Heart jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Mzee Mandela au maarufu kama Madiba historia ya maisha yake ni ndefu, lakini leo katika safu hii tunapenda kushughulika na picha zinazomuonesha akiwa katika vipindi mbalimbali katika maisha yake.
Ila kwa ufupi sana, Mzee Madiba alikuwa mpinzani wa serikali ya kibaguzi nchini mwake, matokeo yake alifungwa maisha katika Gereza la Kisiwa cha Robben lakini akatumikia miaka 27.
Akiwa gerezani, kuna taarifa kuwa Mzee Madiba alitumia blanketi lililotengenezwa nchini Tanzania lenye chapa ya Super Simba na picha ya mnyama huyo (angalia picha).
Kifungo chake kilitokana na kupatikana na hatia ya kuhujumu na kula njama ya kuipindua serikali ya Makaburu. Aliachiwa huru mwaka 1990. Mei 10, 1994 akachaguliwa kuwa rais wa nchi yake akiwa Mwenyekiti wa Chama cha African Congress Party. Juni 14, 1999 aliacha kugombea nafasi hiyo.


Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages