Kama ilivyokuwa kwa Watanzania wengi, usiku wa jana ulikuwa mgumu sana kwangu. Mara nyingi nimekuwa nikiwashangaa mashabiki wa soka wanavyojikuta kwenye huzuni kubwa baada ya timu yao kufungwa.
Wengine hukosa hata hamu ya kula kwa siku kadhaa. Kwakuwa mimi si shabiki wa mpira, sijawahi kupata hisia hii. Lakini hatua ya jana usiku ya Biggie, kumchinjia baharini mwakilishi wa Tanzania wa Big Brother Africa, Ammy Nando aliyekuwa akitegemewa na wengi kuwa mmoja washiriki wanaoweza kuwa washindi wa mwaka huu, ilinifanya nihisi hisia kama wapatazo mashabiki wa soka, huzuni. Ni sababu iliyonifanya jana nilale mapema.
Nando aliondolewa (disqualified) kwenye shindano hilo kwa kuonesha utovu wa nidhamu, kumshambalia na kumtukana mshiriki mwenzie Elikem, na kumtishia maisha.
Ni kweli Nando alistahili adhabu ile na kwa kiasi kikubwa, ametuangusha sana. Japokuwa bado tuna matumaini kwa Feza Kessy, lakini kuondoka kwa Nando kumeiondoa hamu ya si tu Watanzania kufuatilia shindano hilo, bali kwa mashabiki wengi wa nchi nyingi za Afrika waliokuwa wanampenda Nando.
Mbaya zaidi ameondoka kwa sifa mbaya, uhuni, ujana wa kijinga, utoto, usela ma*i, ulimbukeni na hasira za mkizi. Nando alikuwa amebakiza wiki chache tu kufika kwenye mstari wa mwisho wa shindano hilo na huenda maisha yake yangebadilika milele kwakuwa alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda.
Alichokifanya Nando ni sawa na mwanafunzi aliyebakiza wiki mbili afanye mtihani wa taifa halafu anamtukana mkuu wa shule/chuo, usela ma*i haswaaa.
Nando alisahau kuwa ule ni mchezo na hauhusiani kabisa na maisha ya nje. Huenda hakupata muda wa kuzipitia vizuri sheria za shindano hilo, labda asingejiingiza kwenye fujo na uhuni wa aina ile.
Siku zake nzuri na za kuvutia kwenye jumba hilo, zimeharibiwa na dakika chache zilizotiwa dosari na mdomo wake na maamuzi ya kitoto ya kujifanya John Cena ama Floyd ‘Money’ Mayweather.
Uamuzi wa kumpa kibuti Nando, ulichukuliwa na Big Brother kufuatia ugomvi uliozuka Ijumaa hii kati yake na Elikem.
Bahati mbaya ni kuwa Nando ndiye aliyeuanzisha ugomvi huo na hivyo kumfanya avunje baadhi ya sheria za Big Brother.
“Any Housemate who becomes physically violent will be removed from the House immediately. Violence can refer to self-inflicted violence, or violence towards another. Violence includes provocation, goading, bullying and victimisation,” alisema Biggie.
Lakini katika msimu huu, Big Brother alianzisha sheria iliyopewa jina ‘Three Strike Rule’ ambayo itatumika kwa mshiriki atakayefanya kitendo kikubwa cha kuvunja sheria za shindano hilo.
Kutokana na ugomvi huo, Nando alipata Strike yake ya pili huku Elikem akipata moja.
Baada ya hapo, Nando aliitwa kwenye Diary Room na kupewa Strike ya tatu kwa kutishia maisha ya Elikem kwa kusema: “I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die”, (Najiskia kumchoka kisu. Mtu kama huyo anastahili kufa)
Mbaya zaidi ni kuwa, Nando alikutwa akiwa amelala na mkasi chini ya kitanda na hiyo si mara ya kwanza kukutwa akiwa na silaha kwenye jumba hilo. Ni wazi uwepo wa Nando kwenye BBA ulikuwa tishio kwa maisha yaw engine, ni kweli alistahili kutolewa ili kuepusha shari.
Mwezi uliopita alipata Strike ya kwanza na onyo kali kutoka kwa Big Brother baada ya kwenda na kisu kwenye party ya Channel O. Kisu cha nini sehemu kama hiyo? Nando bhanaa.
Umiliki wa silaha ama kusudi la kufanya ukatili kwenye jumba hilo ni kinyume na sheria za Big Brother.
Baada ya Diary session Nando jana, Nando aliambiwa afungashe virago mara moja huku pia Big Brother akitoa onyo kwa washiriki wengine kuishi kwenye jumba hilo kama watu wazima.
Biggie alikuwa na maana kubwa kuwaambia washiriki waliosalia ‘kubehave kama watu wazima’ kwakuwa tabia aliyoionesha Nando ni ya utoto uliopitiliza. Ana miaka mingapi vile?
Itawachukua muda mrefu Watanzania waliokuwa nyuma yake kumsamehe kwa ujinga alioufanya.
Bado haijulikani kama Nando anakuja Tanzania moja kwa moja ama ataenda Marekani alikokuwa akiishi. Kama atachagua kuja kwanza Tanzania, basi ategemee mapokezi hafifu kwakuwa amezivunja roho za watu wengi waliokuwa wakimpenda.
Nando atakuwa na wakati mgumu sana akija kuendelea na maisha ya kawaida kwakuwa amezingua kwa namna nyingi.Usisahau kuwa ana wakati mgumu pia kwa watu wa Ghana kwakuwa atatakiwa kusawazisha scandal yake na aliyekuwa mshiriki wa nchi hiyo, Selly ambaye anamtuhumu kuwa alimwambukiza STD. Kiufupi Nando ni adui mkubwa wa Ghana kwa sasa.
Selly anadai kuwa hakufanya mapenzi na Nando na mama yake amepanga kumshitaki Nando kwa kuchafua jina la bintiye, na ameshawasiliana na watayarishaji wa shindano hilo. Anasema ameshapimwa na wala hana ugonjwa wowote wa ngono na kwamba hajui Nando aliupata wapi ugonjwa huo.
Tusubiri kuona maisha mapya ya Nando akirudi mtaani. Pamoja na kutoka kwa aibu, bado atakuwa na future nzuri kwenye fashion industry barani Afrika na hata kwenye filamu, hasa zile za action!! Lol.
Hizi ni baadhi ya reactions za watu mbalimbali baada ya Nando kuondolewa kwenye shindano hilo.
Jocelyne Maro
If he had stayed composed he definitely would have won…what a wrong way to leave the house…shame…
$un$hine☀
Nando was a weak chap! U don’t brag about stabbing people n think thats strength. Be gone gangsta wannabe Tanzanian #BBATheChase
Godfrey Rugambwa
Nando umetuvua nguo watanzania mbele ya waafrika wote bro! Sasa nchi zote za Afrika zimeelewa kuwa hivyo ndivyo watanzania tulivyo! SAD. Namuangalia Bimp anakusanya kila kilichokuwa cha Kaka yetu (Nando) huku akiwa anahema vibaya sana! The dude is so damn cool All the best bro
KW @keezywear
Nilikuwa naamini Nando angechukua 300 USD za #BBATheChase, but I was wrong… Ungeacha uhuni wako kwa siku chache zilizobaki Nando!!!
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, July 29, 2013
Home
Unlabelled
BIG BROTHER: HIVI NDIVYO NANDO ALIVYOSABABISHWA KUFUKUZWA NA BIG
BIG BROTHER: HIVI NDIVYO NANDO ALIVYOSABABISHWA KUFUKUZWA NA BIG
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.