Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, July 23, 2013

SHANGWE ZATAWALA BIG BROTHER BAADA YA FEZA KUIONA VIDEO YAKE YA AMANI YA MOYO KWA MARA YA KWANZA

Ukiwa ndani ya jumba la Big Brother Africa, ni ngumu kabisa kujua ulimwengu wa nje unaendeleaje. Bahati iliyoje kwa Feza Kessy ambaye weekend hii amefanikiwa kuiona kwa mara ya kwanza video ya wimbo wake, Amani ya Moyo iliyochezwa kwenye kituo cha Channel O.
Baada ya kuchezwa video hiyo, jumba zima lilionekana likiruka juu juu na kupiga vigelegele, shangwe na ndelemo kwa furaha kubwa. Feza Kessy alionekana akizunguka huku na huku kwa furaha tele na kuwakumbatia washiriki wenzake akiwemo Mtanzania mwenzake, Nando aliyekuwa ameshika bendera ya Tanzania. Wengine walimbeba juu juu mrembo huyo aliyekuwa amepoteza maneno ya kuongea zaidi ya kupiga kelele za furaha tu.
Mchumba wake Oneal naye hakuficha hisia zake baada ya kumuona Feza kwa mara ya kwanza kwenye video akiimbia (bila shaka amempenda zaidi kwa hilo). Ni Pokello pekee ndiye aliyekuwa amejitenga pembeni na glass yake ya pombe lakini hakujizuia kutikisa kichwa kufuata mdundo wa wimbo huo.
Ama hakika hiyo ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwa Feza Kessy.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages