Moja ya vitu tofauti katika toleo hilo la ‘Coca Cola Life’ ni sayansi iliyotumika kutengeneza chupa za barafu ‘award-winning PlantBottle’ za soda hiyo zenye uwezo wa kuyeyuka pindi soda inapomalizika, kwa lugha nyingine hakuna chupa ya kutupa inayobaki baada ya soda kumalizika.
Chupa za barafu
Taarifa iliyoripotiwa na Daly Mail, kampuni ya Coca Cola imesema sayansi inayotumia katika utengenezaji wa chupa hizo, ‘Silicone molds’ hujazwa na maji, kisha kuyagandisha kwa digrii -13 Fahrenheit na kuwa barafu, kisha chupa hizo zenye maumbo ya barafu hujazwa na soda ya Coca Cola. Baada ya hapo chupa hizo hubandikwa label yenye logo ya Coca Cola kwa utaalam.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, Coca Cola Life ndio kinywaji cha kwanza kutengenezwa na kampuni hiyo chenye utamu wa asili wa sukari na ‘stevia’, pamoja na calories 108 kwa kinywaji ya chupa ya ml 600.
Kampuni hiyo haijasema kama inampango wa kuzindua kinywaji hicho sehemu nyingine.
Tazama video ya chupa za barafu na jinsi zinavyoweza kuyeyuka baada ya soda kuisha.