Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, August 28, 2013

BAADA YA KUPATANISHWA, HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA NEY WAKATI CHIDI BENZ YUPO SJEJINI

Chidi Benz na Ney wa MitegoUkiniuliza ni stori ipi kubwa toka Serengeti Fiesta 2013 ianze… mpaka sasa hii iko kwenye Top 5, ni kupatanishwa kwa wakali wa hiphop ambao hawakuwahi kuongea wala kukaa sehemu moja.
Beef ya marapa Chidi Benz na Ney wa Mitego ilikua kubwa mpaka kuchanana kwenye nyimbo zao lakini hatimae mwisho wa beef ukawa August 25 2013 kwenye show ya Serengeti Fiesta 2013 Singida.
Kwenye exclusive interview na millardayo.com na AyoTV, Madee ambae ndio aliwapatanisha anasema ‘Ney anaimba nyimbo zake nyingi na ananiimba lakini uelewa wangu uko tofauti sana na Chidi, Chidi anakua kama hataki kuelewa kwamba yule jamaa mipango yake ni biashara ya muziki wake ifanye vizuri, hawezi kufanya kitu kizuri mpaka amtaje mtu na hawezi kukutaja tu we Salum Rajabu… lazima uwe staa’
‘Mimi niliplan kuwakutanisha na yametokea Fiesta na hizi ndio faida tunazizungumzia kila siku ili wanaodhani Fiesta haina faida yoyote waone hii ikiwa mojawapo, maadui wanakua marafiki… pamoja na hizi hela ambazo tunazipata, niliplan kuwapatanisha toka ilipotoka single ya ‘muziki gani’ na Diamond Platnums, ilipotoka Chidi Benz alipanic sana na alikua anafikiria ni ugomvi wa kweli na akawa na hasira lakini Ney hayuko hivyo, anakuimba na mnapiga stori kama kawaida’ – Madee
‘Ni kitu ambacho nilikiona ndio maana sikua na matatizo na Ney akiimba chochote mpaka namwambia kabla hajatoa wimbo ananitumia naisikiliza kama hii iliyotoka sasa hivi kanitumia kabla na nilikua najua mapema Ney atatoa wimbo anasema hivi hivi hivi…… siku ya kwanza ya kuwapatanisha tulikwenda Club tukakuta wasanii wengine wengi wako kimpango wao alafu Chidi yuko mwenyewe na hakuna mtu anaedili nae, Cassim ndio akaniita tukawa pamoja lakini kichwani mpango wangu uleule wa kuwapatanisha’ – Madee
Madee anazidi kutitirika kwamba Dj wa club alipogundua wasanii ‘watoto wa mjini’ wameingia club akaanza kucheza nyimbo mojamoja za wasanii wote aliowaona club ambapo ikafika zamu ya Chidi Benz akapiga Dar es salaam stand up wasanii wote wakawa wanachana akiwemo Ney wa Mitego ambae alicheza pia, Chidi nae kachana alafu mwishoni akainama kama anataka kulia hivi hiyo ni baada ya kuona na Ney anashangilia muziki wake.
Baada ya hapo Madee hakuzungumza chochote kuhusu kuwapatanisha bali walipiga stori nyingine za show ya Fiesta iliyokua inafanyika kesho yake ambapo walipokua backstage kabla ya Ney na Chidi kupanda kwenye stage, Madee ndio akawakutanisha Ney na Madee na kuwapiga picha na kuongea nao kwamba huu ni muziki na ndio maisha yao hivyo hakuna haja ya ugomvi tena ambapo Ney wa Mitego alisema ni kweli yeye anatafuta hela lakini hana matatizo na mtu.
Kilichofata ni kubadilishana namba za simu kwa wakali hawa wawili, wakapeana mikono na bata likaendelea ambapo Chidi Benz alipokua juu kwenye stage Ney alikua anacheza na kuimba nae backstage na vivyo hivyo kwa Chidi Benz.
Hii hapa chini ni video ya backstage ikionyesha jinsi Ney wa Mitego alivyokua akiimba na kuchana baadhi ya mistari ya Chidi Benz aliekua akifanya show kwenye stage ya Serengeti Fiesta 2013 alafu video inayofata ni ya simulizi nzima ya Madee kuwapatanisha.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages