Muigaji wa filamu kwenye orodha A nchini, Irene Uwoya aka Oprah ama Mama Krish ana habari njema kwa Watanzania wenye nyumba mbovu kutokana na umaskini. Kupitia Clouds TV, Irene anakuja na version ya Kitanzania ya ‘Extreme Makeover: Home Edition (EM:HE)’ kwa kukarabati nyumba za wananchi maskini. Kupitia show hiyo iitwayo Paradise, Irene atakuwa akipokea barua kutoka kwa wananchi wenye nyumba chakavu na wale watakaomshawishi nyumba zao zitafanyiwa ukarabati. Kwenye video ya kutambulisha show hiyo, Irene amesema:
“Naitwa Irene Uwoya, wengi wananifahamu kama Oprah kutokana na movie ambazo nimecheza. Mimi ni kioo cha jamii. Mimi kama Irene nilikuwa na wazo langu. Kwa ushauri wangu na maproducer wangu wakanipa mawazo makubwa zaidi. Naamini Watanzania wengi wanaishi kwenye mazingira kama haya. Usisite kuniandikia barua na kunielezea matatizo yako na shida ambazo zinakukabili wewe katika familia yako na nyumba yako.
Mimi kama Irene na crew yangu na watanzania wenzangu tutakusaidia kupitia barua yako. Basi naomba uandike malalamiko yako uniconvince mimi kutembelea nyumba yako nione jinsi gani naweza kukusaidia.”
Mhhh, sounds like a good show!!!