Kuanzia weekend hii watumiaji wa simu zinazotumia Android watakuwa na uwezo wa kutumia huduma ya kutumiana ujumbe ya BBM katika simu zao baada ya kampuni ya Blackberry kuamua kuifanya ianze kupatikana katika simu zinazotumia mifumo tofauti na Blackberry.
Hii inamaanisha sasa watumiaji wa Samsung na simu zote za Android pamoja na watumiaji wa iPhone watakuwa na uwezo wa kudownload ‘app’ ya Black Berry Messenger (BBM) bure na kuchat na watumiaji wa Blackberry. Lakini huduma hiyo haitapatikana kwa watumiaji wa simu zinazotumia Windows. Hapo kabla BBM ilikuwa inapatikana kwa watumiaji wa Blackberry pekee.
Apllication ya BBM itaanza kupatikana katika simu za Android kuanzia kesho jumamosi , wakati watumiaji wa iPhone zinazotumia mifumo ya iOS 6 or iOS 7 wataweza kudownload kuanzia Jumapili hii.
Wataalam wanasema kuwa Blackberry iko katika wakati mgumu kutokana na mauzo yake kushuka na kupoteza soko kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa makampuni pinzani, hivyo inahitajika kufanya kitu kwaajili ya kujiokoa, hivyo hatua waliochukua ni uamuzi sahihi .
kwa mujibu wa Wall Street Journal asilimia 40 ya wafanyakazi wake watapunguzwa kabla ya (2014).
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, September 20, 2013
Home
Unlabelled
HABARI NJEMA: BBM SASA KUPATIKANA KATIKA SIMU ZA ANDROID NA IPHONE
HABARI NJEMA: BBM SASA KUPATIKANA KATIKA SIMU ZA ANDROID NA IPHONE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment