Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, September 21, 2013

MASHUUDA NCHINI KENYA WASEMA WATEKAJI WALIWAACHIA WAISLAMU


Kwa mujibu wa taarifa za sasa, takriban watu 20 wameripotiwa kuuawa na wengine 50 kujeruhiwa wakati ambapo mapambano ya bunduki yanaendelea kati ya polisi na watu hao wenye silaha walioiteka mall ya Westgate jijini Nairobi, Kenya.
article-2427892-1822C8DC00000578-605_638x365
Majeruhi wakisaidiwa kutoka kwenye eneo hilo
Shuhuda mmoja anadai aliwasikia watu hao wakiwaambia waislam wasimame na kuondokoa na kwamba wasio waislamu pekee ndio waliwalenga.
article-2427892-1822BC1B00000578-787_638x390
Majeruhi
Askari wa ulinzi walionekana wakitoa miili iliyotapakaa damu ikiwa imeweka kwenye matoroli ya supermarket.
_70036397_019379281-1
Huduma ya kwanza ikitolewa kwa majeruhi
Balozi wa Uholanzi nchini humo Rob Vandijk ameliambia shirika la AP kuwa alikuwa akipata chakula kwenye mgahawa uliomo ndani ya mall hiyo pindi watu hao wenye silaha waliporusha bomu hilo. Polisi wameizingira mall hiyo na harakati za kuwakomboa watu walioshikiliwa mateka kwenye mall hiyo zinaendelea.
article-2427892-1822C3CD00000578-409_638x397
Askari polisi akijiweka sawa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages