Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, September 24, 2013

TAARIFA KUTOKA KENYA ZINASEMA MWANAMKE ''WHITE WIDOW'' KIONGOZI WA AL-SHABAAB NDANI YA WESTGATE AUWAWA


white-widow
Wakati mapambano bado yanaendelea dhidi ya wanamgambo wachache wa al Shabaab waliobaki ndani ya Westgate Mall, maofisa wa Kenya wamesema angalau al Shabaab watatu wameuawa katika harakati za kuokoa mateka.

Taarifa zinasema mmoja wa magaidi hao ni mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa mwanamke huyo aliyetajwa ni Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White Widow” au “Mjane Mweupe” au “Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha anaripotiwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mume wa Samantha alikua mpiga mabomu wa kujitoa mhanga (suicide bomber) anayeitwa Germaine Lindsayambaye baada ya kusilimu alitumia jina la
Abdullah Jamal alikua ni mmoja wa magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga mabomu ya kujitoa mhanga katika treni tatu na kuua watu 56 nchini uingereza Julai 7, 2005 ambao unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7″
"White Widow" Samantha Lewthwaite na mumewe, 7/7 suicide bomber Germaine na mtoto wao katika picha ya familia
“White Widow” Samantha Lewthwaite na mumewe, 7/7 suicide bomber Germaine na mtoto wao katika picha ya familia
Germaine Lindsay, mume wa "White Widow" wakati wa uhai wakeGermaineLindsay,mumewa“WhiteWidow”wakati wa uhai wake

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages