AZAM TV KUINGIA HEWANI MWEZI UJAO

1377169_224621101037472_893234737_n
Cameraman wa Azam TV akiwa kazini
Ikiwa imeanzishwa mwaka huu pekee, Azam TV imepanga kupanuka zaidi na kuzifikia nchini nyingi za Afrika. Imedai lengo lake ni kuwa na vipindi vya aina mbalimbali kutoka channel za ndani na nje vinavyozifaa familia na watu wa kila rika.
IMG_4592
Pamoja na kuwa na channel zingine zipatazo 50, Azam TV itakuwa na TV zake tatu ambazo ni Azam One itakayokuwa ikionesha vipindi vya Kiafrika hasa vya Kiswahili, Azam Two itakayokuwa ikionesha channel za kimataifa ambapo vipindi vingine vitatafsiriwa kwa Kiswahili.
1383579_224622007704048_940194191_n
Pia kutakuwepo na channel ya Sinema Zetu ambayo itaonesha filamu za Tanzania saa 24.
Kampuni hiyo imejenga studio mbili kubwa zilizopo Tabata ambapo hadi January 2014 zitaanza kurekodi vipindi vya ndani na vya maongezi (talk shows).
IMG_4565
Wafanyakazi wa Azam TV wakiwa pamoja na waandishi wa habari waliotembelea studio zao

Comments