BAADA YA KUZUSHIWA KIFO HATIMAYE CELINE DION AIBUKA HADHARANI NA KUITANGAZA ALBUM YAKE YA '' LOVED ME BACK TO LIFE''

Celine-2
Kwa mujibu wa Mail Online habari hizo za uvumi zilizoenea katika mitandao ya kijamii ya facebook na twitter ziliripotiwa pia na akaunti za vyombo vikubwa duniani vinavyoaminika vya CNN pamoja na FOX News.
Habari hiyo inasema kuwa Jumapili iliyopita CNN walipost taarifa yenye kichwa cha habari ‘R.I.P. Celine Dion 1968 – 2013′ na kueleza kuwa Celine Dion amefariki dunia kwa ajali ya ndege majira ya saa 5 asubuhi siku ya Jumapili, : ‘At about 11 a.m. ET on Sunday, Celine Dion died in a plane crash.’
Celine-1
Habari iliyoripotiwa na FOX yenyewe ilidai kuwa Celine amefariki dunia katika ajali ya gari, nakuongeza kuwa wachunguzi wamewaambia waandishi wa habari kuwa Celine Dion alipoteza control akiwa anaendesha gari la rafiki yake: ‘Investigators have told reporters that Celine Dion lost control while driving a friend’s vehicle on Interstate 80 and rolled the vehicle several times killing her instantly.’
Habari hiyo iliendelea kusema ‘The vehicle was believed to have been traveling at approximately 95mph in a 55mph zone at the time of the accident.’
Celine-3
Celine Dion akisaini autographs kwa mashabiki wake wa New York
Baada ya uvumi huo Celine mwenye miaka 45 ameonekana hadharani Jumatatu ya wiki hii (October 28) jijini New York akiwa mzima na mwenye afya njema na kumaliza kabisa uvumi huo.
Jana Celine alihojiwa na kituo cha NBC alipokwenda kuitangaza album yake mpya ‘Loved Me Back To Life’, na baadaye jioni alisaini autoghraph kwa mashabiki wake wa New York.
Celine-4
Inasemekana hii ni mara ya pili kwa Dion kuzushiwa kifo, mara ya kwanza ilikuwa ni March 2012 alipozushiwa kifo na habari hizo kusambaa kupitia twitter.
Watu wengine maarufu waliowahi kukutwa na R.I.P baada ya kuzushiwa kutangulia mbele ya haki ni pamoja na Kanye West, Justin Bieber, Eddie Murphy, Britney Spears na wengine.

Comments