Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600
wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na
watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni
mwao hakuna viongozi wakuu wa serikali.
Hayo yalibainishwa na Kiongozi wa kundi
la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji
Chande maarufu kama Sir Andy Chande.
Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es
Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya Tanzania kuwa na
wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama duniani inapungua tofauti na
inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno mengi
kuhusu kundi hilo. Alisisitiza kuwa si rahisi kumjua mwanachama wa kundi
hilo, bali wenyewe ndio wanaofahamiana, akisema ni siri na kwamba
wenyewe wanakutana katika vikao mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.
Alisema nchini kuna wanachama zaidi ya
600 wakiwemo wafanyabiashara, watumishi serikalini, walimu pamoja na
wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza kuwa kuna
maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo, ambayo siyo ya kweli.
Alisema idadi ya wanachama wake duniani
inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi sasa wako milioni sita,
tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.
Chande alizungumza na mwandishi wa
habari hizi katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert ambako yeye ni
Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50 tangu
kuanzishwa kwake.
Alisema duniani kuna watu wazito wengi
ambao ni wanachama wa kundi hilo kama majaji wakubwa na hata Binamu wa
Malkia Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi hilo.
Akizungumzia masharti ya kujiunga na
kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama huyo awe anaamini katika
Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au Muislamu.
Alisema pia ni lazima anayetaka kujiunga
awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo hawaruhusiwi
kujiunga na lazima familia ya anayetaka kujiunga na wanandugu wafahamu
kuwa umejiunga na kundi hilo.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, February 21, 2014
TANZANIA INAWACHAMA ZAIDI YA 600 FREEMANSON,.SOMA HAPA UWAJUE NI KINA NANI HAO!!
Tags
WHAT#
Share This
About DARVEL LAMAR BLOG
WHAT
Labels:
WHAT
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment