Mchumba wa Fariq Abdul Hamid, Nadira Ramli.
Mmoja wa rubani wa ndege ya Malaysia iliyopotea, Fariq Abdul Hamid.
Mpenzi
wa kike wa mmoja wa marubani wa ndege ya Malaysia iliyopotea Nadira
Ramli amejichimbia katika hoteli moja jijini Kuala Lumpar na amewataka
ndugu zake kutoangalia televisheni.
Fariq
Abdul Hamid, 27, alikuwa amepanga kumuona msichana huyo ambaye pia ni
rubani msaidizi katika ndege ya shirika jingine. Kwa sasa amepewa likizo
ya mwezi mmoja ili kuiweka akili yake sawa wakati akisubiri matokeo ya
ndege hiyo.
Taarifa juu ya uhusiano huo zilizovuja, zinasema kuwa rubani huyo aliyerusha ndege yenye namba MH370, ana uhusiano na kiongozi mmoja wa upinzani nchini Malaysia aliye jela.
Taarifa juu ya uhusiano huo zilizovuja, zinasema kuwa rubani huyo aliyerusha ndege yenye namba MH370, ana uhusiano na kiongozi mmoja wa upinzani nchini Malaysia aliye jela.
Rubani
huyo msaidizi anachunguzwa baada ya kuwepo kwa habari kwamba yeye ndiye
alikuwa mtu wa mwisho kusikika wiki hii muda mfupi kabla ya mfumo wa
mawasiliano wa ndege hiyo kukatika.
Hamid
alikutana na Nadira walipokuwa wakisoma pamoja chuo cha urubani katika
shule ya Langkawi na wawili hao wamekuwa katika uhusiano kwa zaidi ya
miaka tisa sasa
CHANZO: DAILYMAIL

Comments
Post a Comment