Mtoto Neema Joseph (2) akilia kutokana na maumivu makali ya jicho.
KWELI ni
zaidi ya mateso! Ukisema we unaumwa lakini unapata usingizi, kumbe
hujawaona wagonjwa wenyewe! Mtoto Neema Joseph (2) anateseka kwa
ugonjwa wa jicho ambalo limefumuka na kutoka nje huku likitoa harufu
kali na maumivu yasiyo na mfano,Mtoto huyo anayelia wakati wote
kutokana na maumivu, anaishi na mama yake mzazi, Annastazia Yohana (28)
kwenye Kijiji cha Bugomba, Kata ya Bulungwa wilayani Kahama, Shinyanga.Akizungumza
huku akimwaga machozi kwa uzito wa tatizo la mwanaye, mama Neema
alisema hali yake ya maisha kiuchumi ni mbaya, hasa kufuatia kufiwa na
mumewe, Josephat miezi tisa baada ya kujifungua mtoto huyo huku akiwa
analea watoto wenginewawili.
SIKIA KILIO CHA MAMA NEEMA
“Tangu mume wangu afariki dunia nimekuwa na maisha ya shida, sina
msaada kwani hakuna ndugu wa mume wala wangu wenye hali nzuri ya maisha
na walio tayari kunisaidia kubeba mzigo wa maisha yangu
No comments:
Post a Comment