| Amos Hamis, maarufu kama Anti Asu akimvisha pete mpenzi wake. |
| Anti Asu enzi zake. |
| Anti Asu akipozi na mpenzi wake. |
| Wapenzi hao wakiombewa. |
| Anti Asu akimwinua kidole juu mchumba wake wakati akimvisha pete. |
| Anti Asu akiwa kanisani na mchumba wake. |
| Anti Asu katika pozi lingine enzi zake. |
Stori: Imelda Mtema na Shani Ramadhani - Global Publishers
KATIKA
tukio linalochukuliwa kama ni la kihistoria kuwahi kutokea katika miaka
ya karibuni, shoga wa Jijini Dar es Salaam, Amos Hamis, maarufu kama
Anti Asu, aliyeokoka Agosti mwaka jana, ametangaza nia ya kutaka kuoa
katika Kanisa la TAG, Magomeni wiki iliyopita.
Amosi
alimvalisha pete ya uchumba, Astrida Samatha baada ya kukamilisha
taratibu zote za mila na desturi za ukweni na hatimaye kupewa ruksa ya
kumuoa.
Mara
baada ya misa ya pili kumalizika katika kanisa hilo, Amos alimvisha
pete mchumba wake huyo na kusababisha nderemo na vifijo kutoka kwa
waumini wa kanisa hilo, ambao waliahidi kuchangia baadhi ya gharama
wakati wa harusi yao.
Amos alisema alijikuta akitamani kuwa na mwanamke baada ya kuokoka lakini hakuwa na mawazo hayo kipindi alipokuwa shoga.
Astrida,
mwanamke aliye tayari kuolewa na Amos, alisema Mungu ameagiza upendo wa
dhati ukiwemo ule wa roho, hasa kwa watu kama hawa na siyo vizuri
kuwatenga.
"Tumeagizwa
upendo ule wa roho, mimi naona ni sawa kwa kuwa na yeye ni mtu kama
mimi na anahitaji upendo wa dhati na ninaahidi kumpenda," alisema
Astrida.
Akizungumzia
suala hilo, Amosi ambaye ni maarufu sana jijini Dar es Salaam enzi zake
akijishughulisha na mapenzi ya jinsia moja, alisema:
"Siamini
na wala sikuwahi kufikiria kama nitakuja kuwa na familia yangu,
namshukuru sana baba mchungaji, kwani nina imani hata hao wanaoendelea
na ushoga ipo siku watarejea kwa Bwana."
MCHUNGAJI ANENA
Mchungaji
kiongozi wa kanisa hilo, Dustan Kanamba, alisema Agosti, mwaka jana,
Amos aliamua kuachana rasmi na ushoga na kuokoka, ndipo yeye na mke
wake, walipoamua kumchukua na kuwa sehemu ya familia.
"Mimi
na mke wangu tulishauriana na kumchukua ili awe mmoja kati ya familia
yetu, japo kabla ya kuokoka alikuwa hajisikii kuwa na mwanamke lakini
hali ilibadilika pale alipookoka na kujiona anahitaji kuwa na mwanamke
kwani kwa kipindi cha miaka 29, Amos hakuwahi kumjua mwanamke," alisema
mchungaji.
WAUMINI WAMPONGEZA
Baadhi
ya waumini wa kanisa hilo wamempongeza Amos kwa hatua aliyofikia na
kuahidi kumpa sapoti katika ndoa yake inayotarajiwa kufungwa hivi
karibuni, huku wakitaja baadhi ya vitu watakavyomuwezesha kama kumshonea
suti ya kufungia ndoa na vinginevyo.
Amos
aliachana na mambo ya ushoga Agosti, mwaka jana baada ya kuokoka na
kufanyiwa maombi na mchungaji kiongozi wa kanisa la T.A.G, Magomeni
Mikumi jijini Dar.
Comments
Post a Comment