WERAA! Watu
weweee! Dume lililofahamika kwa jina moja la Lusajo au Sajo anayefanya
kazi maeneo ya Kijitonyama, Dar jirani na duka la mtangazaji Maimartha
Jesse ‘Mai’ amejikuta akitaharuki na kuaibika baada ya kusutwa laivu
katikati ya wanawake huku akilishwa keki na kufunguliwa mvinyo kisa
umbeya, Ijumaa Wikienda limeshuhudia tukio zima.
Kwa
mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wikiendi iliyopita kabla ya
gazeti hili kutua, Maimartha alidaiwa kusuka ishu hiyo huku
akiwakaribisha marafiki zake kushuhudia akiwemo Flora Mvungi.
Ilisemekana
kwamba Mai alidai kuwa kilio chake kwa muda mrefu ni kwamba jamaa huyo
amekuwa akimfuatafuata na kumwambia mumewe, Raymond Shayo ‘Shaa’ kila
jambo analolifanya dukani hapo, ikiwa ni pamoja na kumweleza watu wa
kila aina wanaoingia ndani hapo.
“Nilishapata
taarifa za Sajo kuwa huwa ananichunguza, sikutaka kuwa na haraka
nikaenda naye taratibu bila kumwambia kwani nilikuwa nikimtafutia dawa
ya kumkomesha. Leo ndiyo arobaini yake imefika.
“Nilishika
simu ya mume wangu nikakuta SMS za Sajo zikimuomba fedha, ukweli
nilichukia sana na nilishangaa kuona kumbe kazi anayoifanya ya
kunichunguza analipwa, nikaona sasa ndiyo wakati wa kumkomesha kwani kwa
kulipwa kwake ipo siku atatunga hata uongo kwa sababu fedha ni
shetani,” alisema.
Keki ya msuto aliyoandaliwa Bw. Sajo.
Sajo,
kabla ya kujua kinachoendelea, alikaribishwa keki na shampeini, akaenda
kichwakichwa, alipomaliza kulishwa akaambiwa asome maneno yaliyoandikwa
kwenye keki ‘Sajo acha umbeya ndoa tamu’ ndipo akachanganyikiwa na moja
kwa moja msuto ukaanza huku akiulizwa ni kwa nini anamwambia maneno
mume wa Mai.
“Mh! Mimi mbona siyo kweli jamani,” alisema Sajo na kushindwa kumalizia maneno.
Alipobanwa
na wanahabari wetu na Gea Habibu (wa Leo Tena ya Clouds FM) juu ya kuwa
na namba ya simu ya mume wa Mai, Sajo alishikwa na kigugumizi na
kuondoka ambapo alikimbilia dukani kwake na kujifungia kukwepa aibu
kwani siyo tukio la kawaida kwa mwanaume kusutwa kwa umbeya
No comments:
Post a Comment