Diamond akiwa amevaa nguo ya Roperrope ambayo designer wake mmarekani alidai kuwa ni feki
Devontae Roper, ni designer wa Los Angeles, California, Marekani ambaye ametokea kujipatia umaarufu kwa nguo zake zinazovaliwa na mastaa wa muziki nchini humo wakiwemo August Alsina, YG, Chris Brown, Future na wengine. Brand yake inajulikana kwa jina la RoperRope.
Devontae Roper
Juzi Roper alipost picha ya Diamond Platnumz akiwa amevaa nguo zenye mfanano na designs zake na kumchana staa huyo kuwa ameiba ubunifu wake kupitia yule Diamond aliyemuita kama ‘designer’ wake ambaye kazi yake hasa ni ‘stylist’.
“I usually don’t blast people who make or wear fakes of my designs but this person went way too far when they used my logo! @diamondplatnumz is wearing fake #Roperrope shirt made by a person with bad character and a strong lack or originality! This is not ok! If you steal a design please reframe from using the Designers Logo because it’s illegal www.shoproperrope.com,” aliandika kwenye Instagram.
Post hiyo ambayo hata hivyo tayari imefutwa ilisababisha mjadala mkubwa na wengi iliwafanya wamfahamu Roper ambaye nguo zake zimekuwa zikionekana kwenye video nyingi za August Alsina, Future na Chris Brown.
Wapo waliomshutumu Diamond na kudai kuwa ameumbuka lakini wengi walimtetea na kwa kusema yeye ni mvaaji tu wa nguo hizo na hana kosa hata kama alivaa nguo feki.
Roper alipost picha nyingine ya Diamond na kuandika: Bless Up emoji I just got news #Roperrope just went International emoji God is everywhere #YoungGod x #ICantLose #ShippingOverseas #ThanksEastAfrica #GodFlow @DiamondPlatnumz hit me up next time.”
No comments:
Post a Comment