Malalamiko hayo yalitolewa na meneja wa Diamond, Salam kupitia mtandao wa Instagram:
“iTunes the company below as #Rockstar4000 who act as they have license to sell the songs of my artist @diamondplatnumz on @iTunes they are THIEVES. They don’t have any contract or any relationship with us this is Unacceptable to let companies sell contents of the Artists without any agreement both sides,” aliandika.
“Wizi kwa Wasanii wetu HAUKUBALIKI. Naomba hii Kampuni ya Rockstar4000 iachane na Wizi wake wa kuuza kazi za @diamondplatnumz hatuna makubaliano yoyote na kampuni yako kuuza Nyimbo za @diamondplatnumz Tutakutana Mahakamani. Uvumilivu umetushinda.”
Bongo5 ilimtafuta mkurugenzi wa vipaji na muziki wa Rockstar 4000, Seven Mosha ili kujibu malalamiko ambaye hata hivyo alisema hawezi kulizungumzia hilo na kututaka tumtafute afisa uhusiano wa kampuni hiyo, Lucy Ngongoteke.
- “Hizi taarifa ndo nazisikia naomba tupewe muda wa kulifuatilia, na mimi ndo nalisikia kutoka kwako,” Lucy ameiambia Bongo5. “Ninaomba nifuatilie then nitarudi kwako. Siwezi kuongelea kitu ambacho sina taarifa nacho.
No comments:
Post a Comment