Rais Barrack Obama wa Marekani, tayari amewasili mjini Nairobi.
mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake. Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka. Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini. Obama
anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiri mali
katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.
Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku. Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Baadaye rais huyo atafanya mashauriano na rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi. Siku
yan Jumapili rais Obama atahutubia mkutano wa wakuu wa mashirika ya
kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta kabla ya kuhutubia mkutano
mwingine kwa wakenya wote katika uwanja wa Kasakani.
Obama anatarajiwa kuondoka siku ya Jumapili kuelekea nchini Ethiopia.
Maelfu
ya wakenya wamejipanga kando ya barabara kuu inayotoka uwanja wa ndege
ili kumlaki rais huyo wa Marekani, ambaye anarejea nchini Kenya ambako
babake alizaliwa.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment