Good news mtu wangu, ile collabo ya kundi la Mafikizolo kutoka South Africa na mtu wetu Diamond Platnumz imetoka!
‘Tell Everybody’ ndio njia la wimbo, na ni wimbo ambao ni sehemu ya project ya Umoja wa Mataifa iitwayo UN Sustainable Development Goals (SDGs) Project yenye dhamira ya kupambana kutokomeza umasikini, kurekebisha tabia nchi na kuhamasisha usawa kufikia mwaka 2030.
Wimbo huu umeshirikisha pia wasanii kutoka nchi nyingine za Kiafrika, wapo wakina Yemi Alade kutoka Nigeria, Sauti Sol kutoka Kenya, Toofan kutoka Togo, Becca na Sarkodie kutoka Ghana na of course Diamond Platnumz kutoka Tanzania pamoja na Mafikizolo kutoka South Africa!
Kuna mchanganyiko pia wa lugha mbalimbali kama Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Pidgin na Kizulu... kizuri zaidi ni kwamba kila verse utakayoisikia kwenye wimbo huu basi ujue imeandikwa na msanii mwenyewe!
Hapa ninazo baadhi ya picha za wasanii walioshiriki kufanikisha hii project mtu wangu…
Kama bado hujabahatika kukutana na video ya ‘Tell Everybody’ karibu uitazame hapa chini mtu wangu…
No comments:
Post a Comment