Klabu ya Manchester City ya Uingereza September 19 imeikaribisha klabu ya West Ham United katika uwanja wake wa nyumbani Etihad kucheza mechi ya muendelezo wa Ligi Kuu soka Uingereza… Man City ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani kucheza mchezo wake wa sita wa Ligi Kuu imekubali kipigigo kutoka kwa West Ham United.
Manchester City ambayo iliingia uwanjani ikiwa na rekodi nzuri toka kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu, kwani kabla ya kucheza mechi dhidi ya West Ham ilikuwa imecheza mechi tano na kushinda zote, September 19 imepokea kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa West Ham United, magoli ya West Ham yakifungwa na Victor Moses dakika ya 6 na Diafra Sakho dakika ya 31 ya mchezo huku goli pekee la Man City likitiwa wavuni na Kevin de Bruyne dakika ya 45.
Video ya magoli yote
No comments:
Post a Comment