Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, October 24, 2012

Ndege ya kivita yaua rubani JWTZ



Ndege ndogo ya kijeshi ya mazoezi, (Military training aircraft) namba JW 9129, iliyokuwa ikitumiwa na marubani wanafunzi wa jeshi hilo, baada ya kupoteza muelekeo na kugonga kontena kwenye eneo la uwanja wa ndege wa Julius Nyerere eneo la Airwing Ukonga Jijini Dar es Salaam jana. Mwanajeshi mmoja Kepten Deogratius Magushi, alipoteza maisha wakati yeye na mwenzake Kepteni Feruzi Kwidika, walipojaribu kujiokoa kwa kutumia miavuli ya usalama ambapo Kepteni Magushi alirushwa na kudondoka juu ya paa la jengo moja ndani ya uwanja na kupoteza maisha, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alithibitisha jana. (Picha kwa hisani ya JWTZ)

Ndege ya kivita ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imeanguka na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja na kujeruhiwa mmoja wakati wakiwa katika mafunzo ya kurusha ndege.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, akizungumza na NIPASHE alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana majira ya saa 4:28 asubuhi makao makuu ya kambi ya Jeshi la Anga (Air Wing) eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages