Waziri
wa Sayansi Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akifungua
jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa redio ya jamii ya LOLIONDO FM
wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa redio kijijini Ololosokwani.
Uwekwaji wa redio hiyo ya jamii umewezeshwa kwa ushirikiano kati ya
Airtel na shirika lisilo la kiserikali UNESCO katika kijiji cha
Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Kulia
ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na wa
kwanza shoto mwakilishi wa UNESCO, Bi Vibeke Jensen.
Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akijaribu mtambo wa redio kwa kutangaza moja kwa moja (live) kupitia redio ya jamii LOLIONDO FM mara baada kumalizika kwa hafla ya uzinduzi rasmi wa redio hiyo ya jamii iliyowezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilo la kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliowazunguka wawakilishi wa Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani.
Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ambapo waziri huyo alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa redio ya jamii pamoja na miradi mingine ilikiwemo ujenzi wa nyumba za kimasai za kisasa.
Wadau wawezeshaji wa redio ya jamii ya LOLIONDO FM wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja na waziri wa Sayansi Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa mara baada ya uzinduzi wa redio hiyo kijijini Ololoskwani.

---
Press Release
AIRTEL TANZANIA NA UNESCO WAZINDUA REDIO JAMII LOLIONDO MKOANI ARUSHA
• Lengo ni kufikia maeneo mengi zaidi yenye changamoto za mawasiliano ya Redio nchini
• Maeneo zaidi ya 10 Tanzania bara na kisiwani kufikiwa

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel
ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO kwa pamoja
wamezindua Radio jamii katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo
Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na kufanywa na Waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia Mh Makame Mbarawa.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na kufanywa na Waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia Mh Makame Mbarawa.
Mradi wa Radio za jamii ni program maalum
inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na UNESCO yenye lengo la
kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu,
elimu duni, ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni ,
ukandamizaji wa wanawake na watoto na changamoto zinginezo. Maeneo hayo
pia mbali ya kuwa na changamoto huduma za mawasiliano ni duni na
upatikanaji wa huduma za radio kwaajili ya kuelimisha jamii ni
changamoto kubwa.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa radio hiyo,
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Technologia Mh Makame Mbarawa alisema”
ninawapongeza Airtel na UNESCO kwa jitihada zenu hizi katika kuendeleza
mawasiliano nchini hasa vijijini, mimi nimefurahishwa sana kuona wadau
hawa wanavyojiunga najamii ya kijijini hapa na kuwaunganisha na sehemu
nyingine za dunia kwa kuweka radio hii ya Loliondo FM ili kuwawezesha
kupata habari na taarifa muhimu kwa maendeleo ya taifa”.
Hii ni fulsa ya pekee kwenu wakazi wa
kijiji cha ololosokwani pamoja na vijiji jirani kuinua shughuli zetu za
kiuchumi, kutumia radio hii kutoa maoni na elimu, Naamini vipindi
vitakavyorushwa vitakuwa vimelenga jamii husika na kuwa chachu ya kuleta
ufanisi mkubwa katika mabadiliko na maendeleo kwa ujumla”. Aliongeza
Mbarawa Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurungezi wa Mawasiliano Bi
Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel inajisikia furaha kuwa nafasi ya
kuchangia maendeleo jamii nchini Tanzania, tunaamini kwamba kupitia
redio hii na kwa kupitia mtandao wetu ulioenea zaidi wananchi wamaeneo
haya na vijiji takribani 14 vya jirani watanufaika na kuwepo kwa redio
Loliondo fm hapa ololosokwani. Tunategemea kuona maisha ya ndugu na
jamaa zetu wa jamii ya wamasai na wageni waliopo hapa yakibadilika kwa
kasi katika Nyanja zote”
“sasa Wakazi wa ololosokwani watapata nafasi kwa kupitia radio hii, kutangaza utamaduni wao, kuboresha na kupata uongozi bora, kutangaza biashara zao na kukuza soko huku wakitumia huduma ya Airtel money kupata malipo na kuhifadhi pesa zao kwa usalama zaidi” alisema Singano Singano aliongeza kuwa “Mbali na Radio tumeweza pia kuwawezesha wakazi wa kijijini hapa kupata huduma ya internet kupitia Multimedia center tuliyoijenga na kuiwekea mtandao wetu wenye spidi wa 3.75G, Aliongeza Singano.

Naye mwakilishi kutoka UNESCO bw, Ali-amin
Yusuph alisema “UNESCO inayofuraha kuona mradi wa radio unakuwa na
kuwafikia wananchi wengi nchini kwa ushirikiano wa Airtel, kuwepo kwa
radio hii kutaunganisha wakazi wa Ololosokwani na wale wa maeneo mengine
nchini na dunia kwa ujumla. UNESCO tunayo miradi mingi sana ya kusaidia
jamii na Mradi wa Radio hapa Olosokwani umetusaidia kuona maeneo
mengine mengi ya kuweza kusaidia jamii hii ya kimasai, leo tunayo
miradi mbalimbali tuliyoianzisha hapa ikiwemo Mradi wa Solar (umeme wa
jua) ambao utawawezesha akina mama kupata kipato. kwa kupitia mradi huu
wakazi
wa hapa wamepata sehemu za kuchajia simu zao na kuweza kufanya shughuli zinazohitaji umeme kwa malipo kidogo”.
wa hapa wamepata sehemu za kuchajia simu zao na kuweza kufanya shughuli zinazohitaji umeme kwa malipo kidogo”.
“Halikadhalika tumeweza kurekebisha nyumba
za kimasai na kuzifanya ziwe na muundo wa kisasa unaotoa moshi nje ya
nyumba na kuzifanya ziwe na kiwango bora” Alimaliza kwa kusema
mwakilishi kutoka UNESCO bw, Ali-amin.
Uzinduzi wa kituo hicho cha radio
ijulikanayo kama LOLIONDO FM uliambatana na ugawaji wa vitabu vya
masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kijijini humo kutoka
kwa kampuni ya Airtel ikiwa ni kuwahamasisha wanafunzi wengi kupenda
fani ya sayansi wakiwa tangu wadogo kitu ambacho kitachangia kuongeza
idadi ya wataalamu wa sayansi hapa nchini Airtel kwa kushirikiana na
UNESCO inaendelea na mradi wa radio jamii unaotegemea kufikia maeneo
mengi zaidi nchini ikiwemo Sengerema Mwanza, Karagwe Kagera, Chake
Chake Pemba, Makunduchi Unguja , Pangani Tanga, Kyela Mbeya , na Kalama
Shinyanga.
No comments:
Post a Comment