Askari na wananchi wakitazama kofia ya dereva huyo iliyokuwa imetundikwa juu ya miti.
Mwili wa dereva bodaboda, Abeli Nyunza ukiwa umetupwa katika korongo.
Na Francis Godwin, Iringa
WATU wanaodaiwa kuwa ni vibaka wamemuua kwa kumpiga na kitu kizito
katika paji la uso, dereva bodaboda, Abeli Nyunza eneo la National mjini
Iringa na kumpora pikipiki yake.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Muungano Frelimo mjini Iringa jirani na shule ya msingi Muungano.
Wakielezea juu ya tukio hilo, mashuhuda waliozungumza na mtandao wa http://francisgodwin.blogspot.com/
wamedai kuwa majira ya usiku walisikia mlio wa pikipiki na ghafla
ulizimika na baada ya hapo ilisikika sauti ikiita kwa nguvu Peter! Peter
! mfano wa mtu aliyekuwa akiomba msaada na baada ya dakika kama 10 hivi
ukimya ulitanda na ghafla ulisikika mlio wa pikipiki iliyokuwa
ikiondoka kwa kasi.
Mwenyekiti wa bodaboda mjini Iringa, Macurius Chengulla mbali ya
kuthibitisha kifo cha dereva bodaboda mwenzao huyo bado amesema kuwa
wameweka mkakati wa kuendesha msako ili kuwabana wahusika wa mauaji
hayo.
Chengulla amesema kuwa matukio hayo ya kuuawa kwa madereva bodaboda
kwa manispaa ya Iringa ni tukio la kwanza kwa mwaka huu japo matukio ya
kutekwa na kujeruhiwa yamekuwa yakitokea .
No comments:
Post a Comment