Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys
wakishangilia bao lililofungwa na Mudathiri Yahaya Abbas wakati timu
hiyo ilipopambana na Congo Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika mwakani
nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0. (Picha zote na Habari
Mseto Blog)
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo wakipongezana baada ya mchezo kumalizika.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti
Boys, Hussein Twaha akiwatoka mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika
mchezo wa kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo
zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mchezo huo ulifanyika leo
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys imeshinda
1-0.
No comments:
Post a Comment