Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, November 6, 2012

MAONI YA DIAMOND NA MADEE KUHUSU KUWEKA MAJINA KWENYE GARI BADALA YA NAMBA.



.
Siku tatu zilizopita idadi ya magari ya Watanzania ambayo yameandikwa majina yao badala ya namba imeongezeka kupitia macho yangu.
Huo ni mpango ambao umepitishwa na serikali ambapo unalipia milioni 5 kwa miaka mitatu alafu unaruhusiwa kuandika jina lolote unalopenda badala ya kuweka namba kama kawaida.
Novemba 5 2012 miongoni mwa mastaa wa bongofleva Diamond Platnums na Madee wametoa maoni yao kuhusu kuandika majina yao.

.
Namkariri Diamond akisema “ngoja kwanza tujijenge vizuri kuweka miradi na vitega uchumi kadhaa vya kutuingizia pesa tusifanye tu sifa za kuandika majina mwisho wa siku tukaja kuchekwa kwa sababu unapopata bahati kutoka kwa Mwenyenzi Mungu jaribu kumuonyesha kweli kwamba unaitaka hiyo bahati na unaitumia kwa kitu kizuri sio tena nichezee tu hela nikaandike jina aaaaah, hata kifamilia na watu wengine wakisikia wataona dogo ameshaanza kuwa limbukeni wa vihela viwili vitatu, naukubali mpango lakini nikijaliwa nikipata ya kuweka nitaweka lakini bado”
Madee yeye amesema akiwa na kipato kama hicho ambacho kina uwezo wa kufanya hivyo atafanya kwa sababu kama staa anatakiwa awe na muonekano tofauti anapotembea na anapokaa kwa hiyo atafanya manake ni kitu kizuri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages