WATU wanne akiwamo mwanamke mmoja wanaodaiwa kuwavamia na kuwajeruhi
mapadri wawili kwa risasi na nondo mkoani Iringa, wamekamatwa.
Watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Ismani wanahusishwa na matukio mawili
ya ujambazi uliofanyika katika Parokia za Kanisa Katoliki lililopo eneo
la Kihesa Iringa Mjini na Parokia ya Isimani iliyoko Iringa Vijijini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda aliwaambia waandishi
wa habari ofisni kwake jana kuwa watuhumiwa wote wamekamatwa kufuatia
msako makli uliofanywa na polisi baada ya tukio hilo lililsababisha watu
watatu kujeruhiwa.
Alisema nyumbani kwa mwanamke ndiko walikuta bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayodaiwa ilitumika katika ujambazi huo.
Alisema nyumbani kwa mwanamke ndiko walikuta bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayodaiwa ilitumika katika ujambazi huo.
“Upekuzi uliofanyika nyumba kwa nyumba katika nyumba ya mwanamke
ikipatikana gobore iliyotumika kutekeleza uhalifu huo. Nyumba ya
mtuhumiwa mwingine motto wa mwanamke huyo zilipatikana gorori 37 na
gramu 100 za baruti,” alisema.
Katika matukio hayo watuhumiwa wanadiwa kupora Sh4 milioni na Euro 100,
huku wakiwashambulia kwa mapanga na risasi mapadri wawili, Padri Anjelo
Burgio (66) wa Paroko wa Parukia ya Isamani na Msaidizi wake, Padri
Herman Myala (36).
Mwingine aliyejeruhiwa kwenye matukio hayo ni Mlinzi wa Kanisa la Kiaskofu la Kihesa, Batholomeo Nzigiliwa.
Hali za majeruhi
Kamanda Kamuhanda alisema majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kwamba mlinzi wa Kanisa la Kihesa Nzigilwa hali yake ikielezewa kuwa ni mbaya.
Kamanda Kamuhanda alisema majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kwamba mlinzi wa Kanisa la Kihesa Nzigilwa hali yake ikielezewa kuwa ni mbaya.
Alisema mapadri Burgio na Myala, wote wanaendelea vizuri.
Kamanda huyo alisema kuwa wanaendelea kuwasaka watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo.
Kamanda huyo alisema kuwa wanaendelea kuwasaka watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment