Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza sababu zinazosabisha kukosekana kwa umeme katika jiji la Dar es salaam na maeneo mengine nchini.
Akiongea na Radio One asubuhi ya leo Mheshimiwa Muhongo alisema lilikuwepo tatizo katika mfumo wa gesi ambao umerekebishwa zaidi ya mara tatu na kusabasha gesi kukata.
“Tumeomba wataalamu wetu waangalie na ikiwezekana isitoke, sasa ikishatokea namna hiyo inamaanisha kwamba watumiaji wa gesi wanaendelea kutumia gesi iliyo kwenye hilo bomba, kama nyingine haiji inamaanisha pressure inapungua kwahiyo wanahitaji muda wa masaa ili pressure irudi kuwa sawasawa, “ alisema.
“Tatizo la pili ilikuwa ni kwamba mitambo yetu ile ambayo ilikuwa inatumia mafuta kama unavyojua kwa zaidi ya wiki mbili palitokea mtafaruku mafuta yalikuwa hayapo na kama unavyofahamu mafuta ndo yameanza kufika hata huko mikoani sehemu nyingi mafuta ndo yameanza kuwafikia watumiaji kwahiyo haya matatizo mawili yote tumeyaangalia kwa makini sana nadhani kwasababu ni vitu vinatokea mara kwamara tuna jitaidi visitusumbue tena.”
“Lakini umeme wetu mwingi hautokani na maji sasa hivi hilo ndilo Watanzania wana paswa kufahamu, umeme wetu mwingi unatokana na gesi kati ya asilimia 40 na 60 inategemea na uzalishaji wa siku hiyo ukoje alafu unafuata umeme wa mafuta na mwisho kabisa unafuata umeme wa maji.”
Alieleza kuwa tatizo jingine ni la miundombinu ya kusambaza umeme imechoka na hivyo kuhitaji marekebisho ya mara kwa mara.
“Miundombinu ni kwamba kweli imeshoka inahitaji muda kuweka miundombinu mizuri ambayo ni ya kisasa kwamfano kuna sehemu ambazo sehemu moja ikipata hitilafu karibu wilaya mzima inakosa umeme , saa zingine mkoa mzima kwahiyo hiyo ni miundombinu ya kizamani na hilo tatizo mafundi wa Tanesco wanajitaidi na Tanesco tumewaeleza kwamba wajitahidi sana kuwa wanakagua miundombinu yao na kutengeneza.”
Aliongeza kwa kudai kuwa sababu nyingine kubwa ni wizi wa miundo mbinu ya Tanesco ikiwa pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma na nyaya za umeme.
No comments:
Post a Comment