baada ya kutambulisha jina lake jipya kupitia mtandao wa kijamii wa
twitter, Gucci Mane ameamua kubadili mawazo hayo muda mfupi na kuamua
kurudia jina lake hilo hilo.
Gucci Mane alitangaza kubadili jina na kujiita "Guwop" mapema leo hii,
lakini baada ya muda mfupi alibadilisha mawazo na kuamua kubaki na jina
lake.
rapa huyo kutoka atlanta, Georgia,aliandika kupitia twitter leo hii
kutangaza jina hilo jipya, ambapo aliandika kuwa rasmi ataanza
kujulikana kama Guwop itakapofika tarehe 2 july
"July 2nd I'm officially changing my rap name to Guwop and retiring
the great GucciMane Thanks Fans, for 8 years as Gucci now it's Wop
turn," aliandika
lakini muda mfupi baada ya kubadili jina lake, alirudi na kuandika tena
kuwa atabaki kuwa na jina hili hilo Gucci Mane kwasababu mashabiki wake
wameamua hivyo.
"I am officially NOT changing my name to Guwop it will officially stay
Gucci Mane due to my Fans' response.. Trap House 3 & Juug House July
2" aliandika
Gucci angekuwa mmoja wa ma MC walioamua kubadili majina yao publicly
kama angebaki na wazo hilo, kama unakumbuka Snoop Dogg aliamua kubadili
na sasa anajiita Snoop Lion, Mos Def hivi karibuni kawa Yasiin Bey na N.O.R.E. amekuwa P.A.P.I.
Gucci kwa sasa ameachia mixtape yake mpya Trap God 2 na Free Bricks 2 akiwa na Young Scooter

No comments:
Post a Comment