Imetangazwa
kwenye BBC NEWS WORLD zikithibitisha siku ya Rais wa Marekani, Barack
Obama kuja Tanzaniaitakuwa ni tarehe 1/06/2013
Ikulu yathibitisha ujio wa Rais Obama nchini Na Mwandishi Wetu IKULU imethibitisha ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini mwezi ujao ikiwa ni ziara inayolenga kuimarisha uhusiano mwema kati ya nchi hiyo na Tanzania.
Obama ambaye ziara yake itaanza Juni 26 hadi Julai 3 kwa kutembelea pia Senegal na Afrika Kusini, itakuwa ni ya kwanza kubwa kufanyika Afrika katika kipindi chake cha pili cha uongozi. Katika kipindi chake cha kwanza, alikaa saa chache nchini Ghana.
Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema inamkaribisha Rais huyo ambaye atakuwa Rais wa pili kutoka Marekani kutembelea nchini baada ya George W. Bush aliyefanya ziara Februari 2008.
"Ujio wa Rais Obama unalenga kuimarisha uhusiano mwema kati ya Marekani na Tanzania,” alisema Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
Kwa mujibu wa Rweyemamu, ziara hiyo ni utambuzi wa rekodi nzuri ya Tanzania katika masuala ya demokrasia, utawala bora na maboresho ya kiuchumi.
Katika ziara hiyo, Obama anatarajiwa kukutana na maofisa, wafanyabiashara na viongozi wa vyama vya kijamii.Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, May 22, 2013
Home
Unlabelled
OBAMA KUJA TANZANIA TAREHE 01-06-2013
OBAMA KUJA TANZANIA TAREHE 01-06-2013
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.