Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, June 9, 2013

HII NDIO LIST YA WASHINDI WA TUZO ZA KILI AWARDS 2013

IMG_4289
Naye Ommy Dimpoz ameibuka na tuzo tatu zikiwemo za wimbo bora wa Bongo Pop na wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa kwa hit single yake Me and You. Pia hit yake Baadaye imechukua tuzo ya video bora ya mwaka.
IMG_4325
Licha ya kutokuwepo wala kutuma mwakilishi, Diamond alifanikiwa kushinda tuzo kubwa ya pili kwa usiku huo ya msanii bora wa kiume kwa kuwabwaga Ben Pol, Linex, Mzee Yusuf na Ommy Dimpoz na pia kushinda tuzo ya Msanii bora wa kiume Bongo Flava.
Tuzo za muziki wa dance zilitawaliwa na Chalz Baba wa Mashujaa Band aliyeibuka tuzo mbili za Msanii bora wa kiume Bendi na Mtunzi bora wa mashairi – Bendi.
Usiku wa tuzo za KTMA ulipambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Linah, Amini, Richie Mavoko, Mataluma, Hussein Jumbe, Zahir Zorro, Patricia Hillary na Barnaba. Wengine ni Snura, Godzilla, Mabeste, Madee na Afande Sele.
Host wa tuzo hizo mwaka huu alikuwa ni Zembwele na TJ.
Hii ni list nzima ya tuzo hizo.
Wimbo bora wa mwaka
Dear God – Kala Jeremiah

Msanii bora wa Kiume

Diamond
Msanii bora wa kike
Lady Jaydee
Msanii bora wa kike Taarab
Isha Mashauzi
Msanii bora wa kiume Taarab
Mzee Yusuf
Msanii bora wa kiume Bongo Flava
Diamond

Msanii bora wa kike Bongo Flava

Recho
Msanii bora wa Hip Hop
Kala Jeremiah
Msanii bora wa kiume Bendi
Chalz Baba
Msanii bora wa kike Bendi
Luiza Mbutu
Msanii bora anayechipukia
Ally Nipishe
Video bora ya mwaka
Baadaye – Ommy Dimpoz
Mtunzi bora wa mashairi Taarab
Mzee Yusuf
Mtunzi bora wa mashairi Bongo Flava
Ben Pol

Mtunzi bora wa mashairi hip hop

Kala Jeremiah
Mtunzi bora wa mashairi Bendi
Chalz Baba
Mtayarishaji bora wa mashairi muziki wa kizazi kipya
Man Walter
Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka – Taarab
Enrico
Mtayarishaji wa wimbo mwaka – Bendi
Amoroso
Mtayarishaji chipukizi wa mwaka
Mesen Selekta
Rapper bora wa bendi
Fagasoni
Wimbo bora wenye vionjo vya asili
Chocheeni Kuni – Mrisho Mpoto ft Ditto
Wimbo bora wa bendi
Risasi Kidole – Mashujaa Band
Wimbo bora wa Reggae
Kilimanjaro – Warriors from The East
Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Valu Valu – Jose Chameleone
Wimbo bora wa Bongo Pop
Me an You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee
Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa
Me and You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee
Wimbo bora wa Hip Hop
Nasema Nao – Nay wa Mitego
Wimbo bora wa rnb
Kuwa na Subira – Rama Dee ft. Mapacha
Wimbo bora wa ragga/ dancehall
Predator – Dabo

Wimbo bora wa Taarab

Mjini Chuo Kikuu – Khadija Kopa
Wimbo bora wa zouk rhumba
Ni wewe – Amini
Bendi bora ya mwaka
Mashujaa Band

Kikundi bora cha Taarab

Jahazi Modern Taarab
Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya
Jambo Squad
Hall of Fame – Institution
Kilimanjaro Band wana Njenje
Hall of Fame – Individual
Salum Abdallah

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages