Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 14, 2013

RAILA ODINGA APATA MWALIKO KUTOKA KWA OBAMA ATAKAPOKUJA WAKUTANE TANZANIA

Hivi karibuni kulizuka mjadala juu ya ujio wa Rais wa Marekani Barack Obama nchini Tanzania bila kwenda nchi jirani ya Kenya. Taarifa za sasa inaonekana waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga amepata mwaliko rasmi kutoka kwa Obama kuja kufanya naye mkutano Tanzania.
U.S. President Barack Obama and First Lady Michelle Obama With World Leaders at the Metropolitan Museum in New York
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Daily Post wa Kenya inasema Odinga amepata mwaliko huo kutoka kwa Obama alipokuwa anaelekea Afrika Kusini wiki iliyopita katika World class democracy forum ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika.
Bwana Odinga anatarajiwa kutumia private Jet itakayokodishwa na US State Department kwaajili ya kusafirisha viongozi maarufu akiwemo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan kuja Tanzania.
Rais Obama anategemea kuitembelea Tanzania mwezi ujao (July) ikiwa ni moja ya nchi tatu za Afrika ambazo anategemewa kuzitembelea. Nchi nyingine ni South Africa na Senegal.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages