Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 20, 2013

VIDEO:RIHANNA AMPIGA SHABIKI NA MICROPHONE USONI.

Rihanna ambaye anaendelea na Diamonds World Tour amekamatwa na camera akimpiga shabiki usoni kwa microphone aliyokuwa akitumia katika show yake huko Birmingham, Uingereza (June 17).
riri on stage
Akiwa katika show hiyo Riri alimpiga usoni na microphone shabiki mmoja aliyejaribu kumvuta alipojaribu kusogea eneo walipo mashabiki waliokuwa wakishuhudia onesho lake.
Katika Video clip ya tukio hilo iliyowekwa youtube na shabiki mmoja inamuonesha hit maker wa ‘Diamonds’ akipita mbele ya mashabiki waliokuwa wana scream kwa furaha na wengine wakimshika mkono huku anaendelea kuimba, ndipo alipogeuka kwa hasira na kunyanyua juu mkono wake ulioshika microphone na kumpiga nayo usoni shabiki mmoja aliyemvuta kwa nguvu, Kisha akaendelea kuimba huku anarudi jukwaani akisindikizwa na walinzi wake.
Video clip hiyo ambayo imewekwa pia katika akaunti ya youtube ya CNN imeonesha vizuri kwa kurudia sehemu inayomuonesha Riri akimpiga shabiki huyo na mic. kwa ‘slow motion’
Beyonce ni mwanamuziki mwingine ambaye hivi karibuni alipokuwa katika moja ya show za Mrs Carter World tour, akiwa jukwaani aliacha kuimba ghafla na kumchimba mkwara shabiki mmoja ambaye alimpiga kofi la kalio wakati anapita karibu na mashabiki wakati anaimba.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages