Kwa mara ya kwanza msanii wa kike Recho kutoka THT alipoanza kutoa nyimbo na kusikika, hisia za watu wengi ziliemwendea msanii wa kike Ray C aliyejipatia umaarufu hapa nchini kutokana na uimbaji wake na hususan ‘viuno vyake’ awapo jukwaaji, sababu kubwa ikiwa ni Recho amefanana sana na Ray C sauti, uimbaji, uchezaji wa jukwaani pamoja na muonekano.
Kitu ambacho huenda wengi tulikuwa hatufahamu ni mtazamo wa Ray C juu ya Recho ambaye ni kama mdogo wake kiumri na hata kimuziki hasa kuhusu maoni ya watu wanaosema kua ana mcopy.
Leo (July 22) Ray C ametoa jibu la swali hilo baada ya kupost picha ya Recho (akiwa jukwaani) katika akaunti yake ya Instagram. Baada ya picha hiyo ambayo ilikuwa haina caption mashabiki walianza kutiririka kwa maswali ambayo yalisaidia Ray C kutoa hisia zake juu ya Recho aliyemuita dogo lake. Ray aliandika “Dogo Langu Kazini,kwasababu ananipenda na kunikubali lazma tutaimba wote wimbo mmoja for You guys cz hata mimi penda sauti yake sana!!!!!! Miss Upepo@rachelkizunguzungu”.
Picha ya Recho aliyoipost Ray C
Shabiki mmoja alimuuliza swali Ray C ”getmoo1:Uko tofauti ray c thought ungechukia dogo kukucopy ..she is fine ila copy and paste but huo u regendary..sema ttz mtu akiku copy then akudis”.
Na jibu la Ray C lilionesha kuwa Rehema hana tatizo kabisa na swala la Recho kumcopy “Am happy tht am her @getmoo1 Role Model nafurahi kumuhamasisha nae kuingia kwenye music industry”.
Recho ambaye alianza kufahamika zaidi kupitia wimbo wake wa ‘Kizunguzungu’ alikuja kipindi ambacho Ray C alikuwa amekaa kimya sana hivyo uwepo wake uliwafariji mashabiki wa Ray C waliovikosa viuno vyake vya jukwaani na sauti yake iliyotawala katika chati za bongo flevah miaka kadhaa iliyopita.
Unahisi wasanii hawa wawili wanaofanana kuanzia herufi za mwanzo za majina yao ‘R’, sauti, uimbaji na hata uzungushaji wa viuno jukwaani, wakikaa katika wimbo mmoja itazaa kitu gani? Na ikitokea Collabo hiyo ya Ray C na Recho kwa jinsi unavyowafahamu unahisi nani atamfunika mwenzake?
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, July 22, 2013
Home
Unlabelled
ALICHOKIANDIKA RAYC INSTAGRAM AKIAMBATANISHA NA PICHA YA MSANII RECHO, SOMA HAPA (TUTEGEMEE COLLABO KUTOKA KWAO)
ALICHOKIANDIKA RAYC INSTAGRAM AKIAMBATANISHA NA PICHA YA MSANII RECHO, SOMA HAPA (TUTEGEMEE COLLABO KUTOKA KWAO)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.