Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, July 2, 2013

BIG BROTHER AFRICA:ONEAL AOMBA KUMCHUMBIA FEZA KIKWELIKWELI.

Huenda siku si nyingi tunaweza kuanza kuimba ‘mlisema haolewi mbona kaolewa’ baada ya Oneal kumtaka uchumba wa kweli kweli Feza Kessy.
LgScreen-ShotOnealFeza2_74d1aab9-1a24-4e1d-bbad-f477f8add475_001302150017487
Katika kazi waliyokuwa wamepewa kufanya mjengoni humo, Oneal aliamua kupiga magoti wakati akimwaga sera za nguvu kwa Feza na kumwambia kuwa maisha yake yalikuwa shagala bagala kabla hajakutana na mwakilishi huyo wa Tanzania.
Maneno hayo matamu yalimwingia vyema Feza ambaye alikuwa akitabasamu muda wote kuashiria upendo mzito kwa jamaa huyo wa Botswana ambaye anataka wawe na maisha pamoja siku za usoni.
Wasiriki wengine waliamka na kuwashangalia wapenzi hao kama yalivyo maisha ya kawaida. Kazi hiyo ilionekana kuchukua picha ya ukweli hasa kwa wale ambao wameyaweka wazi mahusiano yao.
Kumbuka Nando ni miongoni mwa washiriki waliotajwa kutoka wiki hii, mpigie kura kumuokoa.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages