Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, July 11, 2013

FLORA AZODOLEWA NA WENZAKE BAADA YA KUSHANGILIA TIMU YA BONGO FLEVA ANAYOCHEZEA MUME WAKE H BABA.




Na Mwandishi Wetu
TIMU ya mastaa waliokuwa wakishabikia timu ya Bongo Movie wamemzodoa mwigizaji mwenzao, Flora Mvungi baada ya kumuona anashabikia Timu ya Bongo Fleva anayochezea mumewe, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’.
Nahodha wa Timu ya Bongo Fleva, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ ambaye ni mume wa Flora.
Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar ambapo mastaa hao waliibua minong’ono mara baada ya kuona Flora anashangilia pindi timu ya Bongo Fleva inashambulia lango la Bongo Movie.
“Mh! Tumekaa naye tukijua ni mwenzetu kumbe hamna lolote, bora tumtenge asituharibie shughuli,” alisema staa mkubwa wa kike aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini.
Baadhi ya mastaa ambao walikuwa wamekaa pamoja katika jukwaa na Flora ni pamoja na Shamsa Ford, Rechael Haule ‘Recho’, Chuchu Hans na wengineo.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages