Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, July 17, 2013

PATRICK NGOWI KUCHUANA NA P SQUARE KUWANIA TUZO ZA YOUNG PERSON OF THE YEAR

Mjasiriamali wa Tanzania na mwanzilishi wa kampuni ya Helvetic Solar Patrick Ngowi ametajwa kuwania tuzo kubwa ya Afrika ambayo Benki kuu ya dunia inazitambua kama ‘tuzo za Nobel kwa Waafrika vijana’.
BFon_z8CcAIxL7p
Ngowi atachuana na vijana wengine 10 wa Afrika wakiwemo mapacha Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square la nchini Nigeria kuwania tuzo ya Young Person of the Year.
“Let’s thank God that we have been nominated.Winning isn’t important. Being recognised in Africa, representing Tanzania is! We exist,” Patrick ameiambia Bongo5.
Wengine waliotajwa ni pamoja na mwanzilishi wa Mara Group, Ashish Thakkar wa Uganda, Grace Ihejiamaizu, Nigeria, Ludwick Marishane – South Africa (22), William Kamkwamba – Malawi (25) na Saran Kaba Jones – Liberia (31).
Wengine ni pamoja na Moctar Dembele – Burkina Faso (22), Fohlabenchi Lily Haritu – CAMEROON (27) na Kariuki Gathitu – Kenya (27).
Tuzo hizo zitatolewa mwezi ujao.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages