Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, July 19, 2013

RIHANNA AMWAGIWA CHIPS JUKWAANI BAADA YA KUCHELEWA KWENYE SHOW.

Mpendwa Rihanna hivi hauamini ule usemi wa ‘malipo ni hapa hapa duniani’?? Inavyoonekana mashabiki wa ‘bad girl’ Rihanna aka Riri wameanza kuchoshwa na tabia yake ya ‘uswahili’ wa kuchelewa kwenye maonesho yake, na safari hii walimuandalia dawa yake kwa kuamua kummwagia chips jukwaani baada ya kuchelewa kufika katika onesho lake la Diamonds huko Manchester, Uingereza Jumanne (July 16) wiki hii.
Rihanna m
Japo akili ya mwimbaji huyo wa Diamonds haikujiongeza haraka kuutumia ule mwamvuli wake maarufu ‘Umbrella’ kujikinga na chips hizo kutoka kwa mashabiki hao ambao pamoja na hasira lakini bado walimngojea kwa hamu.
Rihanna (25) alichelewa kwa saa moja tu, lakini hii si mara ya kwanza kuchelewa katika matamasha yake na kuwafanya mashabiki waliofika kwa wingi kumwona wapandwe na gadhabu. Mwezi (march) mwaka huu alichelewa masaa 2 katika onesho lake la Montreal, Canada na (July 6) akiwa amelewa chakali alichelewa tena masaa mawili katika show yake ya Poland.
Mrembo huyo wa Barbados baada ya kupokea zawadi hiyo (chips) kutoka kwa mashabiki wenye gadhabu akiwa jukwaani alijibu mashambulizi hayo kwa maneno makali “There’s a good crazy and there’s a bad crazy. When you throw s*** up here, that’s an epic fail. I wanna get your gifts but I don’t want you to knock my people out”.
Tazama video ya Rihanna akiongea na mashabiki baada ya tukio hilo
SOURCE:BBC

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages