Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, August 29, 2013

BRAKING NEWS: FRANK RIBERY AKWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA 2012 - 2013.



Franck Ribéry akiwa na tuzo yake.
MCHEZAJI wa Bayern Munich, Franck Ribéry ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012 - 2013. Ribéry amewabwaga wachezaji Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa kupanga makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) kwa msimu huu. Msimu uliopita, Ribéry aliiongoza timu yake ya Bayern Munich kuchomoza na ushindi katika fainali dhidi ya Borussia Dortmund kwenye Uwanja wa Wembley uliopo London, England. Msimu wa 2011/14 tuzo hiyo ilikwenda kwa kiungo wa Barcelona, Andrés Iniesta.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages