Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, August 1, 2013

HII NNDIO BARUA YA WATANZANIA WALIOKAMATWA HONG KONG NA MADAWA YA KULEVYA NA KUWATAJA BAADHI YA VIGOGO NA WATU MAARUFU.,SOMA HAPA.

Hii ni nakala ya barua iliyoandikwa Julai 11, 2013 na mfungwa wa Kitanzania kwa niaba ya wafungwa wengine wa Kitanzania waliofungwa huko Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.

Kama barua inavyoonyesha, nakala zimetumwa kwa vyombo vya habari vya Tanzania lakini bado hatujaisoma hii habari ndani ya vyombo vyetu. Labda bado wanaitafiti na kuthibitisha kama ni ya kweli. Ni vigumu kuthibitisha kama yaliyoandikwa kwenye hiyo barua ni ya kweli lakini nadhani labda ingekuwa vizuri kama vyombo vya habari kujaribu kumwuliza aliyekuwa balozi wetu nchini China, ndugu Phillip Marmo ambaye wafungwa hawa wanadai kwenye barua kuwa alishawahi kuwatembelea huko jela.

Habari kwenye link husika inadai kuwa kuna karibu wafungwa 200 wa Kitanzania waliokamatwa na madawa ya kulevya nchini Hong Kong. Kati ya hao 200, tayari 130 wameshakutwa na hatia na wengine 70 wako mahabusu wakisubiri uchunguzi kukamilika. Inadawaiwa kuwa kati ya Mei and Juni mwaka huu, Watanzania 50 walikamatwa Hong Hong na China kwa kupatikana na madawa ya kulevya. Kwa kawaida wanaokutwa na hatia nchini Hong Kong, wanafungwa kifungo cha miaka 9 kama wakikubali kosa. Wanaokutwa na madawa ya kulevya lakini wakakataa kosa wanafungwa miaka 21 baada ya kudhibitika mahakamani kuwa walikutwa na hayo madawa.

Kama ni kweli, habari iliyopo kwenye hii barua ya Watanzania walioko jela Hong Kong ni mfano halisi wa kinachotokea sehemu nyingine za dunia, kama Afrika ya Kusini na kwingineko. Inategemewa barua hii itasomwa na watu wengi Afrika, hasa Watanzania na itawafanya wengi waache hata kufikiria kuwa punda wa kubebea madawa ya kulevya. Siyo vibaya kama hii barua itaweza kumfanya hata Mtanzania mmoja tuu anayetumika sasa kama punda wa kubebea madawa ya kulevya kuacha kufanya hivyo. Maana kama yaliyoandikwa kwenye hii habari na barua ni ya kweli, basi hali ni mbaya tena sana.

Barua yenyewe hiyo hapo chini. Zipo nakala za aina mbili. Nakala ya kwanza imeandikwa kwa Kiswahili na mfungwa wa Kitanzania kwa niaba ya wafungwa wengine wa Kitanzania huko Hong Kong. Nakala ya pili imetafsiriwa kwa Kiingereza na mfungwa mwingine wa Kitanzania huko huko Hong Kong. Waandishi wa barua wametaja mpaka wahusika wakuu kwenye biashara ya madawa ya kulevya. Kama kweli wanahusika sielewi lakini hawa wanaobeba madawa ya kulevya ndiyo wamewataja
 
SOURCE: MWANAHABARIUSWAZI BLOG

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages